Man United yafanikiwa kutinga ligi ya Europa

Timu ya Manchester United imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza michuano ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.




Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Old Trafford leo, ilikuwa ufanyike juzi lakini ukaahirishwa kutokana na hofu kutegwa kwa bomu kwenye Uwanja huo.
Nahodha Wayne Rooney aliifungia United bao la kwanza akimalizia krosi ya Anthony Martial dakika ya , hilo likiwa bao lake la 100 kufunga Uwanja wa Old Trafford Marcus Rashford kupachika goli la pili na baadaye Ashley Young kumalizia la tatu.
Kwa sasa Mashetani hao wekundu wanaamishia makali yao katika mchezo wa fainali ya FA utakaochezwa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace kwenye dimba la Wembley.
Louis van Gaal, ambaye bado hatima yake haijajulikana ndani ya timu hiyo anataka kuiongoza United kupata taji lake la kwanza tokea walivyoshinda ligi kuu ya England mwaka 2013 chini ya Sir Alex Ferguson.
Man United yafanikiwa kutinga ligi ya Europa Man United yafanikiwa kutinga ligi ya Europa Reviewed by liluo on 10:48:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.