Wanawake wa UKAWA walivyotoka Nje ya Bungeni kisa kuitwa ‘Baby’
Umoja wa Wabunge wanawake UKAWA wametoka nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma baada ya jana Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga kusema kuwa ‘Wabunge wote wa viti maalum CHADEMA ili wapate nafasi hizo ni lazima waitwe kwanza Baby‘
Kauli iliyopingwa na baadhi ya wabunge na kumtaka Naibu Spika kutumia kiti chake ili Mlinga atengue kauli yake, Mlinga alikubali kuitengua lakini Leo Mei 06 2106 hoja hiyo ikarejeshwa tena bungeni kuwa ni kauli ya udhalilishaji kwa wanawake.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee amezungumza nje ya Bunge na kusema..>> ‘Jana mbunge Goodluck Mlinga wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria alisema Wabunge wote wa viti maalum Chadema ili apate nafasi za kuwa Wabunge ni lazima awe Baby wa mtu‘
‘Sisi ni wajumbe wa umoja wa wanawake, tunajua nchi hii ina mfumo dume, lakini jana wakati wabunge wanawake wanadhalilishwa kuna wabunge wanawake haohao walikuwa wanapiga makofi ‘
‘Tumewaambia viongozi wetu na tumekubaliana kama wabunge wote kuwa tunaenda kuandika barua kujitoa kwenye chama cha Wabunge Wanawake‘
Wanawake wa UKAWA walivyotoka Nje ya Bungeni kisa kuitwa ‘Baby’
Reviewed by liluo
on
7:56:00 AM
Rating:
No comments: